Afrika yashuhudia wimbi la tatu la COVID-19
share Print Shirika la afya duniani WHO, lImesema Alhamisi kwamba Afrika sasa inashudia wimbi la tatu la maambukizi ya Covi-19 na kwamba idadi ya maambukizi imeendelea kupanda kwa wiki tatu mfululizo,wakati kesi 474,000 zikiripotiwa kuanzia Juni 20. Shirika hilo limeongeza kusema kuwa maambukizi ya sasa yanaenea kwa haraka kuliko wimbi la pili lililoanza mwanzoni mwa mwaka. WHO linasema kuwa hali hiyo huenda imesababishwa na kutozingatia kanuni zilizo wekwa, ongezeko la mikusanyiko pamoja na aina mpya ya virusi vya corona. Aina mpya ya virusi kwa jina delta,vilivyo gunduliwa kwa mara ya kwan...