Zimbabwe yakanusha nia ya kupeleka ndovu China
Zimbabwe yakanusha nia ya kupeleka ndovu China 16 Julai, 2021 Shirikisha share Kundi moja la mazingira la Zimbabwe limeishitaki serikali kutokana na mpango wake wa kupeleka ndovu nchini China. Kundi hilo Advocates4Earth, linailaumu China kwa kuweka ndovu kwenye mazingira hatari kiafya. Katika hati ya mashitaka iliowasilishwa mbele ya mahakama kuu, Advocates4Earth linaomba mamlaka ya kitaifa ya wanyama pori ya Zimbabwe izuiliwe kupeleka ndovu nchini China. Lenin Tinashe Chisaira ambaye ni kiongozi wa Advocates4Earth anasema kuwa wanacho lenga ni kuomba mahakama itoe amri kwamba serikali ya ...