Wake wa marais: Mfahamu Bi Jeanette Nyiramongi Kagame mke wa rais wa Rwanda Paul Kagame
Wake wa marais: Mfahamu Bi Jeanette Nyiramongi Kagame mke wa rais wa Rwanda Paul Kagame Dinah Gahamanyi Chanzo cha picha, Rwanda FirstLady /Twitter Maelezo ya picha, Jeanette Kagame Ni watu wenye ushawishi katika uongozi wa kila siku wa nchi zao, hata hivyo si kila siku utasikia juu ya maisha yao na vipawa vyao. Hawa ni wenza wa marais, ambao baadhi yao ni wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa bega kwa bega katika safari za kisiasa za wenza wao mpaka kushika hatamu za madaraka. Wiki hii tunakuletea mfululizo wa makala kuhusu wenza wa marais katika eneo la Afrika Mashariki na leo tunakupak...