Je ungependa kwenda anga ya mbali? Nauli ni dola milioni 28
Je ungependa kwenda anga ya mbali? Nauli ni dola milioni 28 Saa 6 zilizopita Maelezo ya picha, Jeff Bezos (pichani), kaka yake Mark, na mshindi wa mnada na mtalii mwingine ambaye hajatangazwa wataunda vikosi vinne vya kwenda navyo safari ya Julai 20 Mzabuni ambaye jina lake halijafahamika amelipia dola milioni 28 kwa ajili ya kupata kiti katika chombo cha anga cha Blue Origin kinachomilikiwa na muasisi wa kampuni ya mtandaoni ya Amazon. Mshindi aliyeshinda mnada huo siku ya Jumamosi , hakutajwa jina bali kampuni ya Blue Origin iliandika kwenye kurasa ya tweet kuwa itamtangaza hivi karibuni. ...