Maelfu waandamana Ulaya kupinga vizuizi vya Covid-19 | IDHAA YA KISWAHILI | DW
Maelfu waandamana Ulaya kupinga vizuizi vya Covid-19 Maelfu ya raia kwenye mataifa kadhaa ya Ulaya waliandamana siku ya Jumamosi kupinga vizuizi vya kudhibiti kusambaa ugonjwa wa Covid-19 na sera za kuwalazimisha kudungwa chanjo. Maandamano mjini Paris Wengi walioandamana wanadai sera hizo zinatishia uhuru wa raia katika wakati serikali barani Ulaya zinazidisha shinikizo dhidi ya watu amabo hawajapatiwa chanjo. Nchini Ufaransa, kiasi watu 160,000 walijitokeza kuonesha ghadabu zao dhidi ya rais Emmanuel Macron na serikali yake mjini Paris na katika miji mingine. Muswada mpya wa sheria chanzo ...