Jovenel Moïse: Mjane wa rais wa Haiti azungumza kwa mara ya kwanza
Jovenel Moïse: Mwili wa rais wa Haiti 'ulichanika' kwa kumiminiwa risasi nyingi-mkewe asema Saa 8 zilizopita Chanzo cha picha, Martine Moise/TWITTER Mjane aliyejeruhiwa wa rais wa Haiti ameelezea wakati wauaji "walipommiminia risasi" mumewe baada ya kupenya na kuingia nyumbani kwao katikati ya usiku. Martine Moïse alisema shambulio hilo lilitokea haraka sana, mumewe Jovenel hakuweza "kusema hata neno moja". Rais Moïse aliuawa mnamo Julai 7, ikidaiwa na mamluki 28 wa kigeni. Bi Moïse pia alijeruhiwa katika shambulio hilo, na alisafirishwa kwenda Miami kwa matibabu. Jumamosi, alitoa ujumb...