Mil 600 Zatengwa Simba Kuimaliza AS Vita
Mil 600 Zatengwa Simba Kuimaliza AS Vita
UNAAMBIWA Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameamua kuichukulia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita kama fainali na kuna mzigo ambao umetengwa.
Taarifa za ndani zinadai kuwa hadi kufikia sasa kuna mamilioni ya fedha yametumika na mengine yatatumika ambapo jumla ni shilingi milioni 600 ili kuongeza motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi kama watafanikiwa kuvuna pointi tatu.
Jioni ya Jumamosi, Simba inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, kuwakabili AS Vita Club ya DR Congo kwenye mchezo wa marudio ikiwa na kumbukumbu ya kuvuna pointi tatu kwenye mechi ya kwanza ya ugenini.