Covid-19: Nini kimebadilika Tanzania tangu kifo cha Magufuli?
Covid-19: Nini kimebadilika Tanzania tangu kifo cha Magufuli? Na Peter Mwai Maelezo ya picha, Serikali sasa imekiri kwamba corona ipo na ni tatizo Rais Samia Suluhu alichukua hatamu za uongozi Tanzania takriban miezi mitatu iliyopita kutoka kwa John Magufuli, aliyefahamika sana kwa kutilia shaka mambo mengi kuhusu corona. Rais Magufuli alifariki dunia mwezi Machi kutokana na matatizo ya moyo, na kifo chake kilitoa fursa ya kuwepo mtazamo mpya katika vita dhidi ya Covid-19. Je, Tanzania imebadilika kwa kiasi gani tangu kuondoka kwa Magufuli? Rais Samia amesema nini kuhusu Covid? Kuna tofaut...