vimarsana.com

Page 349 - Carousel Constructor Plugins News Today : Breaking News, Live Updates & Top Stories | Vimarsana

Manara awavaa Yanga Malalamiko ya nini wakati hyo saa moja tutacheza wote?

Manara awavaa Yanga Malalamiko ya nini wakati hyo saa moja tutacheza wote?  Wakati Yanga wakiwa tayari wameshawasili uwanjani na wakijipanga kuanza kupasha misuli. Msemaji wa Simba Haji Manara ametoa kauli kwamba wao wapo tayari kucheza na Yanga muda wowote. Kupitia ukurasa wake wa instagramu Manara ameandika; Malalamiko ya nn wakati hyo saa moja tutacheza wote? Hata cc hatukufurahia mabadiliko hayo ya ghafla , lakini hatuna budi kukubaliana na uamuzi wa Mamlaka !! Simba ipo tayari kucheza hata usiku wa manane, as longer us TFF na Wizara wamesema, We are Ready,,,,Raha ya kiporo ukile usiku kabla kukuchwa Au kama vp suseni tu kama ilivyo ada yenu wazee wa kulalamika hovyo hovyo

Barbara: Bila Kuifunga Yanga, Ubingwa Hautanoga

Barbara: Bila Kuifunga Yanga, Ubingwa Hautanoga MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amefunguka kuwa watafanya kila namna leo, Yanga afe pale kwa Mkapa kwani hakutakuwa na raha ya kuchukua ubingwa pasipo kumfunga mtani wao huyo.   Barbara alisema anaamini kwa asilimia 100 kuwa ushindi utapatikana kwani morali na ari ya wachezaji ipo juu sana na wao kama viongozi wameshamaliza majukumu yao, hivyo kilichobaki ni wachezaji kumaliza kazi ndani ya uwanja.   Akizungumza na Championi Jumamosi, Barbara alisema kuchukua ubingwa ukiwa umemfunga mtani kunakuwa na raha na furaha ya kitofauti, hivyo ubingwa wao wa msimu huu hautakuwa na maana kama watafungwa au kutoka sare na Yanga.

WHO yatoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya China

WHO yatoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya China Shirika la afya ulimwenguni WHO limeidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya Covid-19 iliyotengezwa na kampuni ya China ya Sinopharm.  Uamuzi huo utawezesha mamilioni ya dozi kuweza kuzifikia nchi zenye uhitaji kupitia mpango wa kimataifa wa usambazaji chanjo.  Timu ya washauri wa WHO, imesema hatua hiyo inafungua uwezekano wa chanjo ya Sinopharm kujumuishwa katika mpango wa COVAX katika wiki chache zijazo na kusambazwa kupitia ofisi za kanda za WHO na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.  Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhahom Ghebreysus amesema hatua hiyo inaongeza orodha ya chanjo ambazo COVAX inaweza kuzinunua na kuzipa nchi ujasiri katika kuagiza na kusimamia chanjo. 

Rais Kagame kuwa wa kwanza kuleta kiwanda chanjo ya corona Afrika

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema Taifa lake litakuwa la kwanza kuleta chanjo ya mRNA barani Afrika wakati Afrika ikipambana na janga la virusi vya corona. “Rwanda inafanya kazi na washirika ili kuwa ya kwanza kutengeneza chanjo ya mRNA barani Afrika,” Kagame katika mkutano wa kwenye mtandao wiki hii katika mkutano ulioitishwa na jopo huru la kukabiliana na janga la corona ingawa hakutoa ufafanuzi. Waziri wa Afya wa Rwanda, Luteni Kanali Dk.Tharcisse Mpunga ameliambia Shirika la utangazaji la Rwanda kuwa mjadala huo ulikuwa ni wa kuleta kiwanda cha chanjo Rwanda. “Hii inaweza kuwa hatua kubwa kwa Rwanda na Afrika kupata chanjo…tunategemea kuwa punde mijadala hii itazaa matunda,” Dk. Mpunga amesema Alhamisi usiku.

Critically endangered antelope makes debut at Polish zoo - EXCELSIO | News & Information

Critically endangered antelope makes debut at Polish zoo Critically endangered antelope makes debut at Polish zoo May 07, 2021 Excelsio Media Share To: A critically endangered mountain bongo, born two weeks ago at Warsaw Zoo in Poland, enjoyed a walk outside with its mother. Share

© 2025 Vimarsana

vimarsana © 2020. All Rights Reserved.