Mke wa rais: Mfahamu Angeline Ndayubaha Ndayishimiye mke wa rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye Dinah Gahamanyi Imeboreshwa 19 Julai 2021, 11:09 EAT Chanzo cha picha, Angeline Ndayizeye Ni watu wenye ushawishi katika uongozi wa kila siku wa nchi zao, hata hivyo si kila siku utasikia juu ya maisha yao na vipawa vyao. Hawa ni wenza wa marais, ambao baadhi yao ni wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa bega kwa bega katika safari za kisi a sa za wenza wao mpaka kushika hatamu za madaraka. Wiki hii tunakuletea mfululizo wa makala kuhusu wenza wa marais katika eneo la Afrika Mashariki tukianza na mke wa Rais wa Burundi.