Mpango mpya wa kuwarejesha masomoni wanafunzi waliopata mimba Tanzania utafanikiwa? Saa 6 zilizopita Maelezo ya picha, Karibu watoto 5,000 nchini Tanzania wanatarajiwa kunufaika na mpango wa elimu kwa mfumo usio rasmi katika awamu za mwanzo Serikali ya Tanzania imetangaza mpango mpya wa kuwarejesha masomoni mabinti waliopata ama wanaopata ujauzito wakiwa mashuleni, mpango ambao utaanza ramsi kuanzia mwaka 2022. Chini ya utaratibu wa kuboresha elimu ya sekondari Tanzania (SEQUIP), mabinti hao sasa watapata nafasi ya kuendelea na masomo yao waliyokatisha katika mifumo wa elimu wa kawaida. April mwaka jana, Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ilisema tu wanafunzi watanufaika na utaratibu wa SEQUIP, licha ya kugusia lakini haikuwa bayana kwamba wanaopata ujauzito watakuwa sehemu ya wanafukaika hao.