Baada ya Marekani kuondoa Majeshi yake Afghanistan haya ni maswali 10 kuhusu vita vya miongo miwili Afghanistan
Vita ya Afghanistan: Baada ya Marekani kuondoa Majeshi yake haya ni maswali 10 kuhusu vita vya miongo miwili 9 Julai 2021, 07:30 EAT Chanzo cha picha, BBC/Getty Images Maelezo ya picha, Marekani imekuwa ikipigana Afghanistan tangu shambulio la kigaidi la mwaka 2011 lililofanyika katika ardhi yake Baada ya mzozo wa miaka 20, Marekani imeondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan. Kwa Marekani na washirika wake, kambi ya Bagram ya jeshi la anga ilikuwa kitovu cha vita dhidi ya Taliban and al-Qaeda. Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani viliingia nchini humo Disemba mwaka 2001, na kambi h...