Lazarus Group: Mjue Park Jin-hyok mdukuzi sugu wa 'jeshi la wadukuzi' wa Korea kaskazini
Lazarus Group: Mjue Park Jin-hyok mdukuzi sugu wa 'jeshi la wadukuzi' wa Korea kaskazini 2 Julai 2021, 06:32 EAT Chanzo cha picha, Getty Images Anayatumia majina matatu - Park Jin-hyok, Pak Jin-hek na Park Kwang-jin.Lakini hakuna hakikisho kwamba yote ni majina yake halisi kwa hivyo usiyaamini . Mwaka wa 2016 wadukuzi wa Korea Kaskazini walipanga wizi wa $ 1bn kwenye benki ya kitaifa ya Bangladeshi na nusura watoroke na fedha hizo . Hata hivyo walifaulu kukwepa na dola milioni 81 . Kikosi cha wadukuzi wanaoungwa mkono na Korea Kaskazini kina mwanamme mmoja ambaye anatumia majina mbali mbal...