Marekani yatuma wataalam Haiti
Marekani yatuma wataalam Haiti Shirikisha Print Marekani Jumapili imetuma timu ya kiufundi nchini Haiti kutathmini hali ya usalama na mahitaji mengine baada ya mauaji ya rais Jovenel Moise wiki iliyopita. Haikuelezwa wazi ni taasisi zipi zimeshirikishwa, lakini timu hiyo inapanga kuwasilisha ripoti kwa rais Joe Biden itakaporudi nyumbani, kabla ya maamuzi kuchukuliwa juu ya kuhusika zaidi kwa Marekani katika mzozo mbaya unaokikumba kisiwa hicho cha Caribbean, afisa mwandamizi ameambia shirika la habari la Reuters. Awali, Marekani ilitupilia mbali ombi la Haiti la kuitaka kusaidia kuzima gha...