Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 30.07.2021: Grealish, Pogba, Lukaku, Dest, Lukaku, Trippier, Ederson, Willian
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 30.07.2021: Grealish, Pogba, Lukaku, Dest, Lukaku, Trippier, Ederson, Willian Saa 7 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Aston Villa wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo na kiungo wa England Jack Grealish, 25, wiki ijayo na wako tayari kumpa mkataba mpya wa kuzuia hamu kutoka kwa Manchester City. (Express na Star) Mabingwa wa Ligi ya Premia City, hata hivyo, wameanza mazungumzo na Villa kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo - na uamuzi kuhusu ikiwa makubaliano ya Grealish yanaweza kuafikiwa utafanywa ndani ya siku chache. (Guardian) Meneja wa Manchester Ci...