Mwanza: Askofu Mwamakula, Lwaitama na Wengine 127 Watiwa Mbaroni
HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 128, akiwemo Askofu Emmaus Mwamakula, Dkt. Lwaitama pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa, mkoa na wilaya wa CHADEMA wakati wakijiandaa kuhudhuria kongamano la kudai Katiba Mpya. Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika leo, Julai 17, 2021 katika Hoteli ya Boma, Nyakato jijini Mwanza lakini siku moja kabla ya kufanyika, Jeshi la Polisi lilimuandikia barua Katibu wa Vijana wa Chadema, Wilaya ya Ilemela na kumtaarifu kwamba hawakuwa wametoa taarifa wala kupata kibali cha kufanya kongamano hilo. Katika barua hiyo...